Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepokea jumla ya shilingi milioni 826 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari wilayani humo.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Chiza Marando amezitaja shule Shule zilizonufaika na fedha hizi ni pamoja na Shule ya Sekondari Nandembo, Shule ya Sekondari Tunduru, Shule ya Sekondari Masonya, Shule ya Sekondari Mataka, Shule ya Sekondari Matemanga, Shule ya Sekondari Tarajali Kata ya Mbatin a Shule ya Sekondari Tarajali Kata ya Ngapa
“ Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya elimu wilayani Tunduru, fedha hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari’’,alisema Marando.
Ametoa rai kwa wataalamu,wasimamizi wa miradi na wakandarasi waliopata zabuni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa ubora na kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.