Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Kanali Thomas Laban amesikitishwa na tabia ya baadhi ya Wazazi na walezi kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani hali inayosababisha kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Kanali Laban ameeleza masikitiko yake baada ya Watoto watatu tu wenye ulemavu wa viungo kupatikana katika Wilaya nzima yenye shule zaidi ya 100 kupokea msaada wa viti mwendo vilivyotolewa na serikali kwa lengo la kuwawezesha wenye ulemavu kuhudhuria masomo.
Hafla ya kukabidhi viti mwendo hivyo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ambayo ilihudhuriwa na watoto wenye ulemavu,wazazi wao,walimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya nyasa Jimson Mhagama na wadau wengine wa elimu akiwemo Afisa Elimu Msingi na Afisa Elimu Maalum.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.