SERIKALI kupitia TAMISEMI imetoa pikipiki kwa ajili ya maafisa watendaji kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Akikabidhi pikipiki hizo kwa watendaji wa kata ,Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Ng’waniduhu Malenya aliwaambia watendaji wa kata hao kuwa Serikali imedhamiria kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia watendaji wa kata pikipiki ili kurahisisha usafiri wa kuwafikia wananchi kiurahisi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Malenya alidai ipo mifano katika mikoa mingine watendaji wa kata waliopatiwa pikipiki kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wanatumia pikipiki hizo tofauti na malengo ya serikali.
Malenya aliwataka watendaji wa kata waliopatiwa pikipiki hizo kufanyia kazi za serikali kama ilivyokusudiwa na kinyume cha hapo serikali ya wilaya itafuatilia kwa makini kuhakikisha pikipiki hizo zinafanya kazi ya kusafiria kwenda kutatua kero za wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo katika kata zao.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile alimwambia mkuu wa wilaya kuwa, kata zilizopendekezwa kupata pikipiki hizo ni kata ya magazine,kata ya Lusewa,Kata ya Msisima ,Lisimonji,Mputa pamoja na kata ya Kitanda.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kassimu Gunda aliwahatarisha watendaji wa kata kuwa wasitumie pikipiki hizo kusafirisha nyumba ndogo kwa kuwatumia vijana hali ambayo itasababisha ndoa zao kugundua kuwa pikipiki hizo ndio chanzo cha maovu na kuibua hasira za kukata matairi ya pikipiki hizo na kusimamisha shughuli za kutatua kero za wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo.
Gunda Alisema madiwani watafuatilia katika kata zao kuhakikisha pikipiki hizo zilizotolewa na serikali na kupewa watendaji wa kata zinafanya kazi zilizokusudiwa na sio vinginevyo alisema makamu mwenyekiti huyo.
Ambokile aliongeza kuwa sababu ya kupendekezwa kwa kata hizo ni kutokana na changamoto za miundombinu ya barabara zilizopo katika kata hizo ,katika kuwafikia wananchi wa vijiji vya kata na kuwarahihishia watendaji wa kata kutembelea vijiji na kusimamia shughuli za maendeleo.
Mtendaji wa kata ya Magazini Musa Ponera pamoja na kuishukuru Serikali kwa kumpatia pikipiki hiyo alisema kata ya magazine ipo umbali wa zaidi ya kilomita 200 kutoka makao makuu ya Halmashauri ,kupewa kwa pikipiki hiyo imemrahihishia usafiri wa kufika makao makuu ya Halmashauri kwa shughuli za kikazi pamoja na kutembelea vijiji vya kata yake kutatua kero za wananchi na kusimamia maendeleo na kuhaidi kuitunza pikipiki hiyo ili aweze kufanyakazi iliyokusudiwa na serikali alisema Ponera
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina jumla ya kata 21 ambapo kata 6 kati ya hizo zimepata pikipiki katika mgao huu wa awamu ya kwanza na kubakia kata 15 ambazo watendaji wake watapata katika awamu zijazo .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.