• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatoa sh.bilioni 3.12 kujenga madarasa 156 Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: October 4th, 2022

SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 3.12 KUANZA UJENZI WA MADARASA 156 RUVUMA

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa  shilingi bilioni 3.12 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea katika kikao kazi cha maelekezo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023.

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichowashirikisha watendaji ngazi ya Mkoa na  wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma,Kanali Thomas amempongeza Rais kwa jitihada zake za kuhakikisha anaondoa tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari.

“kwa mara nyingine tena Mkoa wetu umepokea shilingi bilioni 3.12 kutoka kwa Mhe.Rais kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 katika shule za sekondari,ujenzi unatakiwa kukamilika Desemba 15,2022 ambayo ni sawa na siku 75 tu hivyo hatuna budi kufanya kazi usiku na mchana’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Ili kuhakikisha majengo hayo yanakamilika kwa wakati,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameagiza wilaya zote kuimarisha dhana ya ushirikishwaji na uwajibikaji,Halmashauri zote kuunda kamati za usimamizi wa miradi na kuanza mchakato wa manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa mafundi wenye uwezo.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza usimamizi na ufuatiliaji wa ngazi zote ufanyike ili kuhakikisha miradi  hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki amesema Mkoa wa Ruvuma kupitia Mamlaka ya Serikali za Mitaa TAMISEMI umepokea kiasi cha shilingi bilioni 3.12 kutoka serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 katika shule za sekondari 68.

Ameyataja maelezo mahususi ya utekelezaji wa mradi huo kuwa ni kufuata mwongozo wa force account katika utekelezaji wa mradi na kutumia ramani ya darasa iliyoelekezwa kwenye program EP4R na UVIKO 19.

Maelekezo mengine ameyataja kuwa ni kuhakikisha ujenzi unakamilika ifikapo Desemba 15,2022 na utekelezaji wa miradi yote uzingatie thamani ya fedha na ubora wa miradi.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma anayeshughulikia Mipango Jumanne Mwankoo amebainisha kuwa kati ya shilingi bilioni 3.12 zilizotolewa,Manispaa ya Songea imepokea shilingi bilioni 1.52 kwa ajili ya kujenga vyumba 76 vya madarasa.

Mwankoo ameitaja Halmashauri ya Mbinga Mji kuwa imepokea  shilingi milioni 220 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 11,Halmashauri ya Namtumbo imepokea shilingi milioni 340 kwa ajili ya kujenga madarasa 17 na Halmashauri ya Nyasa imepokea sh. Milioni 240 kwa ajili ya kujenga madarasa 12.

Kulingana na Katibu Tawala huyo,Halmashauri ya Songea ,Halmashauri ya Mbinga, na Halmashauri ya Madaba kila mmoja imepokea shilingi milioni 200 kwa ajili ya kujenga vyumba kumi vya madarasa.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Odo Mwisho amewashauri watendaji kuhakikisha wanajenga madarasa hayo katika ufanisi na viwango vinavyolingana na fedha zilizotolewa na serikali na kwamba mapungufu yaliyojitokeza kwenye madarasa ya UVIKO yasijirudie tena.

Katika Mwaka wa fedha 2021/2022,Mkoa wa Ruvuma ulipokea sh.bilioni 10 kupitia fedha za UVIKO zilizowezesha kujenga vyumba vya madarasa 500 katika shule za msingi na sekondari.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma

Oktoba 4,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.