Serikali imetoa shilingi milioni 161 kwa ajili ya kutekeleza Ujenzi wa madarasa mawili ya Awali, na Nyumba ya Walimu yenye uwezo wa kuchukua familia mbili katika Shule ya Msingi Lumeme Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Khalid Kharif amesema ujenzi huo upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji kwa upande wa vyumba vya madarasa mawili ya awali ya mfano umefikia asilimia 98,nyumba ya Walimu asilimia 85 na madawati 60 yamekamilika.
“Wananchi wamehamasishwa na wameshiriki kufanya kazi za kukusanya mchanga, mawe kokoto na tofali kwa kazi zote ambazo wameshiriki kuzifanya zina thamani ya kiasi cha fedha zaidi ya Tshs. Milioni 4”, Amesema Kharif.
Hata hivyo, ameishukuru serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwaletea fedha za mradi huo.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.