Awali akitoa semina kwa kamati hizo Afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya mji mbinga Bi Cecilia Mbata amewaamashisha wananchi kijitolea, kupokea,na kuthamini miradi hiyo ili kuleta chachu kwa selikari kuendelea kuleta fedha kwaajili ya miradi ya maendeleo katika kata zao.
Utololewaji wa semina elekezi kwa watendaji ,na kamati mbali mbali, za usimsmizi wa ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo, vyumba vya madarasa kwa shule za msingi, maabara kwa shule sekondari na Zahanati katika kata 12 za halmashauri ya mbinga mji. Umepata mwitikio mkubwa baaada ya wananchi kujitokeza na kuunda kamati hizo ili kushiriki na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Hatahiyo Serikali kupitia halmashauri hiyo imetoa zaidi ya shilling milioni 442 ili kuakikisha miradi hiyo inakamilika kwa kwakati, ambapo milioni 150 kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati 3,na milioni 292 kwajili ukarabati wa vyumba vya maabara 4 na vyumba vya madarasa 9 .
Semina hiyo imetolewa kila kata kupitia baadhi ya wataalamu wa idara mbalimbali, ikiwemo Maendeleo ya jamii, idara Fedha,Takukuru, Mipango,Ujenzi na kitengo cha Manunuzi. Awali wataalamu hao wamehainisha katika utekelezaji wa miladihiyo , uundwaji wa kamatihizo za ujenzi, wameweka bayana kuwa watendaji wenyeviti wa vijiji na madiwani hawataruhusiwa kua miongoni mwa kamati hizo, hivyo kubaki kuwa wasimamizi na washauri katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Niutaratibu kwa muujibu wa kanuni ya 167 kanuni ya ununuzi wa uma ya Mwaka 2013. Force Account ni njia ya ununuzi inayo tumika kwenye ujenzi ambao utekelezwa na taasisi kwa kutumia wataalamu na vifaa vyake au wataalamu wa ndani lenye lengo la kupunguza gharama za ujenzi na ukarabati na kufanya utekelezaji wa mradi kukamilika kawa wakati, pasipo kuathili utendaji wa kilasiku wa taasisi wakati ujenzi unaendelea .
Wataalamu katika semina hiyo wa wamesistiza kamati hizo kufuata maelekezo waliowapa, kulingana na majukumu ya kila kamati yalio hainishwa katika miongozo ya utekelezaji wa miradi hiyo. Aidha wameongeza kuwa kila kamati katika kila kata kutoa taarifa ya maendeleo ya miradi kila hatua inayofikiwa katika mihutasari ya kila kikao, ikiwemo upokeaji na ukaguzi wa vifaa, manunuzi na katika kamati ya ujenzi maelekezo ya ujenzi hatua kwa hatua.
Aidha wameongeza kua utunzaji wa kumbukumbu zikiwemo nyaraka za manunuzi, zabuni, mikataba, hati ya kukamilisha kazi, mapokezi na nyaraka za malipo mbalimbali ni muhimu kuhifadhiwa, hii pia itasaidia kutathmini thamani ya fedha ya ukarabati na ujenzi halisi. (Value for Money)
Kwa upande wake msimsmizi wa seminahiyo, Mkurugenzi katika Halmashauri hiyo Bi: Grace Quintine amesema fedha zimetolewa na serikali ni kwajili ya kumalizia ujenzi na si vinginevyo hiyo kuwaomba wanakamati kuwaamasisha wanachi na kujitolea ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Imeandikwa na Afisa Habari Mbinga Mji
Aprili 10,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.