SERIKALI imeupandisha hadhi msitu wa Matogoro(Forest Reserve) uliopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kuwa Msitu wa Hifadhi wa asili (Nature Reserve).
Mkoa wa Ruvuma sasa unakuwa na misitu ya hifadhi ya asili miwili yaani Mwambesi wa Tunduru na Matogoro wa Songea ambayo yote ipo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Msitu wa Matogoro uliyopo katika Manispaa ya Songea upo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ,msitu huu ni kivutio adimu cha utalii lakini pia msitu huo chanzo cha mito miwili maarufu nchini.
Chanzo cha kwanza kilichopo kwenye msitu huo chanzo cha mto Ruvuma wenye urefu wa zaidi ya kilometa 800 ambao ni maarufu barani Afrika unaomwaga maji yake Bahari ya Hindi lakini pia mto huo unaunganisha nchi za Tanzania na Msumbiji.
Milima hiyo pia ni chanzo cha Mto Luhira ambao unatengeneza mto Ruhuhu unaomwaga maji yake ziwa Nyasa.Mto Ruhuhu unachangia asilimia 20 ya maji katika ziwa Nyasa.
Hifadhi ya Msitu wa milima ya Matogoro ilianzishwa miaka ya 1950 ikiwa na hekari 2259 za miti ya kupandwa.Msitu wa milima ya Matogoro kisheria upo chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na ulitangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1951.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.