SERIKALI ya mkaoa Ruvuma imewataka Wakulima wa zao la tumbaku kutumia mifumo rasmi wa stakabadhi ghalani ili kuweza kuepukana na changamoto zinazojitokeza wakati wa mauzo wa zao hilo
Akizungumza katika kikao cha kawaida cha mwaka cha Wajumbe wa chama kikuu cha ushirika Songea-Namtumbo (SONAMCU) kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Jeremiah Sendoro, kilichofanyika katika ukumbi wa Chandamali Manispaa ya Songea machi 30,2023
Sendoro amesema Serikali ipo pamoja nao ili kuhakikisha ushirika unaimalika vile vile na wanufaike kupitia umoja huo na kwa upande wa Serikali itaendelea kusimamia mifumo iliyopo ya stakabadhi gharani ikiwa pamoja na kuziondoa changamoto zinazo hikabiri mifumo
“Nawapongeza viongozi wa SONAMCU wakiongozwa na Bodi ya wadhamini kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha chama chetu kinakuwa na wakulima wananafuaika kwenye mazoa ya tumbaku Soya pamoja na ufuta hii yote nakutokana na huimarishwaji wa mfumo wa stakabadhi ya ghara” amesema Sendoro.
Hata hivyo ametoa wito kwa makampuni ambayo yanakuja kununua tumbaku ameyaomba yakawe mabalozi kwa makampuni mengine ili nayo yaweze kuja mkoani Ruvuma katika uzalishaji na ununuzi wa mazao hayo
“Naomba sana tumbaku yetu muinunue vizuri ili Wakulima wetu waweze kunufaika na mwisho kabisa mtusaidie kufufua kiwanda chetu cha Tumbaku hapa Songea maana kimesimama kwa muda mrefu bila kufanya kazi” amesisitiza Sendoro
Naye Mkuu wa Wilaya wilaya ya Namtumbo Mhe, Ngollo Ng’waniduhu Malenya amesema Mkoa wa Ruvuma unarutuba ya kutosha na ndio mkoa pekee ambao unaweza kulima aina nne za tumbaku kwa msimu mmoja hivyo amewataka wakulima kuongeza uzalishaji zaidi ili kukuza vipato vyao
“Wataalamu wanasema heka moja uzalisha kilo 1000 lakini kwa masikitiko kilo 600 ndio zinaingia sokoni kwa maana tunapoteza kilo 400 hili nijukumu letu wote tukiungana tunaweza kuhakikisha kwamba tuaongeza uzalishaji zaidi wa zao hili la tumbaku” amesema Malenya.
Kwa upande wake meneja wa SONAMCU Juma Mwanga, amemshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji hasa katika kilimo cha tumbaku katika uongozi wake wa miaka miwili madarakani wawekezaji wengi wamekuja na uzalishaji umeongezeka Zaidi
“Chama kikuu cha ushirika SONAMCU kinatarajia kuzalisha tani 8000 hii niongezeko kubwa la uzalishaji wa tumbaku kulinganisha na misimu minne iliyopita ambayo wakulima waliweza kuzalisha tani 1000 tu kutokana na juhudi za Serikali inapelekea Mkoa wetu kwenda kuzalisha zaidi msimu huu wa 22/23” amesema Juma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.