SERIKALI imetoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Namtumbo mkoani Ruvuma.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma, Msimamizi wa Ujenzi Mustapha Issa Ponera amesema mradi huo utagharimu kiasi cha fedha shilingi milioni 100 ambazo zimetoka Serikali kuu pia mradi upo hatua za mwisho kukamilika.
Akifafanua kuhusu hatua za ujenzi huo zinavyoendelea, amesema jengo hilo limeezekwa, limepigwa lipu, uwekaji wa fremu za milango unaendelea,utengenezaji wa Grill za madirisha umekamilika na aluminium zimewasilishwa 14 kati ya 20 ambazo zimetakiwa.
“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za mradi huu ambao utawasaidia watoto wenye mahitaji maalumu kuwa katika mazingira bora yenye usalama”, amesema Ponera.
Hata hivyo amesema mpaka sasa kiasi ambacho kimetumika ni zaidi ya shilingi milioni 97 na kilichobaki ni zaidi ya shilingi milioni mbili ambacho kitatumika kwaajili ya ufungaji wa milango mitatu mikubwa na madirisha mawili ya alminium.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya ameahidi kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika na kuanza kuwahudumia wananchi
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.