Mbinga, Ruvuma – Serikali ya Wilaya ya Mbinga imewataka walimu kujiepusha na masuala ya siasa wanapokuwa kazini na badala yake kuzingatia sheria, kanuni, na miongozo ya sekta ya elimu ili kuepuka migogoro na athari kazini.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, alitoa kauli hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Mbinga, uliofanyika katika ukumbi wa St Kiliani, Mbinga Mjini.
Makori alisema walimu wanapaswa kujitathmini kila siku kuhusu mchango wao katika taaluma badala ya kujiingiza kwenye siasa zisizo na tija.
Alisisitiza kuwa walimu ni msingi wa maendeleo ya taifa, na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha sekta ya elimu na mazingira ya kazi ya walimu.
Alieleza kuwa Serikali inafanya juhudi za kuboresha maslahi ya walimu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapandishwa madaraja kwa wakati kulingana na mwongozo wa utumishi wa umma.
Aidha, Makori aliwasihi walimu kushirikiana na Serikali katika kuinua sekta ya elimu, kuendelea kujiendeleza kitaaluma,
Katika hatua nyingine, aliziagiza Halmashauri za Wilaya na Mji wa Mbinga kutumia mapato ya ndani kulipa madeni ya walimu ili kuongeza motisha kazini na kuinua kiwango cha taaluma mashuleni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.