• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SH.milioni 220 zilivyofungua barabara ya Njambe-Ndonga ziwa Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: November 1st, 2022

WAKAZI wa kijiji cha Ndonga kata ya Liwundi Halmashauri ya wilaya Nyasa mkoani Ruvuma,wameishukuru serikali kwa kujenga barabara mpya inayounganisha kijiji hicho na Njambe ambayo imesaidia kuondoa kero za muda mrefu zilizosababishwa na kukosekana kwa barabara ya uhakika.

Wamesema hayo jana mbele ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas, aliyefika katika kijiji hicho kwa  ajili ya kukagua ujenzi wa barabara inayoanzia kijiji cha Njambe hadi Ndonga yenye urefu wa km7.

Barabara hiyo inajengwa na Wakala wa Barabara za mjini na vijijini(Tarura) kwa gharama ya zaidi ya Sh.milioni 220, ambapo  itaharakisha shughuli za uchumi na uzalishaji mali hasa kusafirisha dagaa kutoka ziwa nyasa kwenda maeneo mengine ya Tanzania.

Marietha Mkondola alisema, katika kijiji hicho hakukuwa na huduma yoyote ya mawasiliano ya barabara tangu uhuru mwaka 1961,badala yake wananchi walipotaka kusafiri kwenda maeneo mengine wakiwamo watumishi wa umma walilazimika kutumia mitumbwi na boti  hali ambayo imechelewesha sana uchumi wao.

Mkondola alisema,kukamilika kwa barabara hiyo sasa kutasaidia hata makazi yao hasa ardhi kuwa na thamani kubwa na kuongezeka kwa idadi ya watu watakaokuwa wanaitumia kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidan Mbele alisema,tangu serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani mwaka mmoja uliopita,wameshuhudia maendeleo makubwa  katika kijiji chao ambapo serikali imejenga na kuboresha huduma za kijamii ikiwamo umeme na barabara.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas,ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeiangalia barabara hiyo kwa jicho la pili kwani wananchi walikuwa wanapata changamoto kubwa ya usafiri pindi wanapohitaji kwenda maeneo mengine.

Alisema,serikali inafanya kazi kubwa ya kutatua kero mbalimbali katika sekta ya barabara,umeme na nyingine kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kujenga na kukarabati barabara kwa lengo la kurahisisha huduma ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa ili kukuza uchumi.

Alisema,kijiji hicho kilikuwa kama kisiwa kwa sababu kukosekana kwa mawasiliano ya barabara ambapo alitolea mfano,kwenda makao makuu ya kata Liundi walilazimika kutumia mitumbwi ambayo wakati mwingine haikuwa salama.

Amewataka wananchi wa kijiji cha Ndonga kutambua kuwa barabara hiyo ni yao,hivyo wana wajibu wa kuilinda  kwa ari na mali ili iweze kudumu kwa muda mrefu na waitumie kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo.

Kanali Laban,amemuagiza Meneja wa Tarura wilaya ya Nyasa  Mhandisi Thomas Kitusi, kuhakikisha inafanya marekebisho kwa baadhi ya maeneo ambayo yatajengwa makalavi.

Meneja wa Tarura wilayani Nyasa Thomas Kitusi alisema,Barabara  hiyo inaunganisha kata ya Kihagara na Liwundi hadi sasa wametumia kiasi cha Sh.milioni 220,305,000.00 kuifungua barabara hiyo katika kipindi cha miaka miwili ambapo awali  katika kijiji hicho hakukuwa  na mawasiliano yoyote ya barabara.


Alisema,tangu uhuru barabara hiyo haikupitika na hivyo wananchi wa kijiji hicho hawakuwahi kuona gari,na usafiri pekee ulikuwa mitumbwi na boti  na kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha ambazo zimetumika kufungua barabara hiyo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.