• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SHULE hii haipo Ruvuma,serikali yaonya wanaosambaza uzushi

Imewekwa kuanzia tarehe: June 19th, 2025

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imetoa tamko rasmi ikikanusha vikali taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye mitandao zinazodai kuwepo kwa shule ya msingi iitwayo “Madaba” yenye changamoto kubwa za miundombinu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo akizungumza na wanahabari kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas, amesema, shule hiyo haipo kwenye orodha ya shule zilizosajiliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, na haijawahi kuwapo katika rekodi za Serikali.

Amesisitiza kuwa taarifa hizo, zina lengo la kuchafua taswira ya Serikali, na kwamba zimesababisha taharuki kwa wananchi, hasa wazazi na wadau wa elimu.

Hata hivyo  amesema upotoshaji huo si mpya kwani hata mwaka 2022 video feki hiyo iliwahi kusambazwa ikionesha wanafunzi wakisomea chini ya kibanda cha miti katika shule inayoitwa Litapatile, ambayo pia haipo katika Wilaya ya Madaba wala mkoani Ruvuma.

“Mwaka 2022 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alikanusha hadharani taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari baada ya kufanya uchunguzi wa kina. Tunaendelea kusisitiza kuwa hakuna shule yoyote yenye jina la Madaba au Litapatile katika orodha ya shule zilizosajiliwa mkoani Ruvuma,” alieleza Bi. Makondo katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Katika kuhimiza uwajibikaji na uadilifu wa kihabari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetoa wito mahsusi kwa waandishi wa habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanafanya uhakiki wa kina kutoka pande husika kabla ya kusambaza taarifa kwa umma.

Taarifa zisizokuwa na uthibitisho zimeelezwa kuwa zinavuruga amani na juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Aidha, Ofisi hiyo imetoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na kusambaza taarifa hizo za uongo, ikibainisha kuwa ni kosa la jinai chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao Na. 14 ya mwaka 2015, ambapo yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini, ambapo baadhi ya watu wasio waadilifu wamekuwa wakitengeneza na kusambaza taarifa za kughushi kwa malengo ya kisiasa, kibiashara au kuvuruga amani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UJENZI wa barabara ya kihistoria Tanzania na Msumbiji kuunganishwa kwa lamii kupitia Songea

    June 21, 2025
  • MADABA yafunguka ,uwekezaji wa bilioni 20 waleta mapinduzi katika afya na elimu

    June 21, 2025
  • HALMASHAURI Ruvuma zaagizwa kutekeleza HOJA za CAG

    June 20, 2025
  • SHULE hii haipo Ruvuma,serikali yaonya wanaosambaza uzushi

    June 19, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.