• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SHULE mpya za sekondari za kata 184 kujengwa

Imewekwa kuanzia tarehe: January 8th, 2023

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -T AMISEMI anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde amesema katika mwaka wa fedha 2022/23, Serikali inatarajia kujenga shule mpya za sekondari za kata 184 huku kila halmashauri ikipata shule moja.

Shule hizi zinajengwa kupitia awamu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekodari (SEQUIP).

Dkt. Msonde ameeleza hayo Januari 6, 2023 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika Halmashauri ya Namtumbo Mkoani Ruvuma ya kukagua shule maalum ya wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kupitia Mradi wa Kuboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika mwaka wa fedha 2021/22  tayari zimejengwa shule 232 za kata na mwaka huu wa fedha kabla ya kufika mwezi Juni 2023, tutakuwa tumekamilisha ujenzi wa shule mpya 184 za kata, na kiła halmashauri itapata shule moja," amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde ameeleza kuwa ujenzi wa shule za sekondari za kata utaenda sambamba na ujenzi wa shule mpya 5 nyingine za wasichana za sayansi zinazopaswa kujengwa kila Mkoa.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa shule za wasichana za sayansi ilihusisha ujenzi wa shule 10  ambazo ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji kwa gharama ya Sh. bilioni 30.

Aidha, Dkt. Msonde amefafanua katika ujenzi wa shule za sekondari za kata utagharimu Sh milioni 600 kwa kila shule lakini awamu ya kwanza ya ujenzi Serikali inatoa Sh. milioni 470 kwa kila shule na Sh. milioni 130 zitatolewa katika awamu ya pili ambazo zinatumika kujenga nyumba za walimu na kununua vifaa vya TEHAMA vya kujifunzia.

Wakati huo huo, amewatoa hofu wazazi kwa kueleza kuwa Serikali imeweka jitihada kubwa ya kuboresha shule zote za kata kwa kuboresha miundombinu ili kuwapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari kwa kujenga Shule ya Sekondari kila kata.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • SEKONDARI ya Dkt.Samia alama ya maendeleo Namtumbo

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.