MKOA wa Ruvuma umetisha kwa Utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Jamii (COVID -19) na kufikia asilimia 96.
Hayo amesema Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde mara baada ya kukagua miradi hiyo na kuangalia viwango vya ujenzi amesema Ruvuma ipo mbele akilinganisha na Mikoa mingine.
’’Sina cha kusema nampongeza Mkuu wa Nkoa,Ma DC,Wabunge pamoja na watumishi wote kwa kusimamia vizuri Miradi ambayo hata Rais Samia amehimiza,nina waahidi kuwaletea miradi mingine’’.
Silinde amesema mwaka 2022 wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza madarasa na madawati yanawasubilia,imekuwa tofauti na miaka mingine wanafunzi walikuwa wanasubilia madarasa yajengwe kupitia nguvu za wananchi ili waanze masomo.
Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Ruvuma Juma Fulluge amesema ujenzi wa Miradi ambayo ni asilimia 80 ya Madarasa yaliyojengwa yatasaidia kuondoa changamoto ya Wanafunzi kukosa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2022.
Fulluge amesema Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na asilimia 20 ya Madarasa na Upungufu ulikuwa asilimia 80 ambapo Serikali imejenga Madarasa 448 kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.
Amesema mwaka 2021 walifanya mtihani 39,614 na wamefaulu 29, 314 sawa na asilimia 74 na kutarajia kujiunga kidato cha kwanza kwa wakati kupitia Madarasa yaliyojengwa na kuondoa upungufu wa Vyumba vya Madarasa.
,,Mkoa umepokea fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Jamii kiasi cha Shilingi Bilioni kumi laki tatu ishirini elfu kwaajili ya Vyumba vya madarasa 448’’.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkoa wa Ruvuma
Desemba 17,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.