SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kuleta simba wawili jike na dume katika bustani ya wanyamapori Ruhila Manispaa ya Songea kabla ya Sikukuu ya pasaka mwaka huu..
Antony Masebe ni Kamanda wa Kituo Kidogo cha Kanda Kusini Mashariki amesema utengenezaji wa vibanda maalum vya kuwahifadhi Wanyama hao (cages) kwenye bustani hiyo umekamilika.
Amesema simba hao tayari wamechukuliwa katika hifadhi moja mkoani Arusha na kuanza safari ya kuwaleta hapa Songea na kwamba wakati wowote wanawasili kwenye bustani ya wanyamapori Ruhila.
Ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kuhakikisha katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka wakiwa na familia zao wanafika kufanya utalii wa ndani katika bustani ya Ruhila iliyopo kilometa saba tu kutoka katikati ya mji wa Songea
Amewataja Wanyama ambao wanapatikana katika bustani hiyo kuwa ni pundamilia, pofu, kakakuona, kuro, swalapala, sungura, nyumbu,jamii ya nyani ambapo amesema bustani hiyo ina madhari ya kuvutia ikiwemo maeneo ya michezo ya watoto,maeneo mazuri ya kupigia picha na kuweka kambi kwa ajili ya utafiti
Amekitaja kiingilio katika bustani hiyo kuwa ni shilingi 2,360 kwa mtu wa kuanzia umri wa miaka 18,chini ya miaka 17 ni shilingi 1180 na kwa Watoto chini ya miaka mitano wanaingia bure.
Bustani ya asili ya Ruhila ambayo ipo chini ya TAWA ilianzishwa mwaka 1973 na imekuwa inapokea watalii wa aina mbalimbali kutoka ndani ya nje ya nchi.
Imeandikwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.