• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SIMBA wawili Lucy na Liana kuchochea utalii wa ndani Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: April 7th, 2023

 SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii  imeleta  simba wawili majike wanaitwa Lucy na Liana katika bustani ya wanyamapori  Ruhila Manispaa ya Songea  mkoani Ruvuma ili kuchochea utalii wa ndani.

Akizungumza kwenye hafla ya upokeaji wa simba hao iliyofanyika ndani ya bustani ya Ruhila mjini Songea, Mkuu wa Utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa  Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Kusini Mashariki Kamishina Msaidizi Said Mshana  amesema simba hao wametoka hifadhi ya wanyamapori  ya  Sevo jijini Arusha.

“Hawa simba kule sevo wildlife  watu walikuwa wanapiga nao picha na kuwakumbatia ndiyo hawa,sasa sisi tukaona ngoja tuwalete Ruvuma na tumeamua wabaki kama simba ili kuchochea utalii wa ndani kwa watu wa Songea ambao kwa muda mrefu waliomba tuwaletee simba’’,alisema Kamishina Mshana.

Akizungumza  kwenye hafla hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Ndile ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea ameipongeza TAWA kwa kuleta simba hao katika bustani ya wanyamapori Ruhila ambapo amesema simba hao watawahamasisha wananchi kupenda kufanya utalii wa ndani,

 Amesema kuwa bustani hiyo ni kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla ambapo amesema huo ni mkakati wa serikali ya Mkoa wa Ruvuma  kumuunga mkono Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo amesema mji wa Songea sasa utachangamka katika sekta ya utalii.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano  ameipongeza TAWA kwa kuleta Wanyama hao ambapo amesema sasa wananchi wa mji wa Songea wamepata sehemu maalum ya mapumziko  hivyo ametoa rai kwa wananchi kumiminika katika bustani ya Ruhila.

Amesema mji wa Songea una bahati kwa kuwa na bustani ya asili ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo katikati ya mji na kwamba serikali imeiboresha bustani hiyo ambayo hivi sasa ina wanyamapori wengi wakiwemo simba,nyumbu,pofu na pundamilia.

Amesema Manispaa ya Songea imemuunga mkono mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maeneo ya vivutio vya utalii ambapo amesema katika Manispaa ya Songea kuna  vivutio vingi vikiwemo bustani ya Ruhila,Makumbusho ya Taifa ya Majimaji na chanzo cha Mto Ruvuma kilichopo milima ya Matogoro.

Antony Masebe ni Kamanda wa  Kituo Kidogo cha Kanda Kusini Mashariki amesema  watalii wa ndani katika bustani ya wanyamapori Ruhila wanaendelea kuongezeka ambapo takwimu za mwaka huu zinaonesha  kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu jumla ya watalii 750 wametembelea bustani ya wanyamapori Ruhila.

Ametoa rai kwa wananchi wa Songea katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka kufika kufanya utalii wa ndani katika bustani hiyo ambayo hivi sasa ina wanyamapori wa kuvutia wakiwemo simba pundamilia, pofu, kakakuona, kuro, swalapala, sungura, nyumbu,jamii ya nyani na ndege ambapo amesema bustani hiyo ina madhari ya kuvutia ikiwemo maeneo ya michezo ya watoto,maeneo mazuri ya kupigia picha na maeneo ya kuweka kambi kwa ajili ya utafiti

Amekitaja kiingilio katika bustani hiyo kuwa ni shilingi 2,360 kwa mtu  wa kuanzia umri wa miaka 18,chini ya miaka 17 ni shilingi 1180 na  kwa Watoto chini ya miaka mitano wanaingia bure.

Bustani ya asili ya Ruhila ambayo ipo chini ya TAWA ilianzishwa mwaka 1973 na imekuwa inapokea watalii wa aina mbalimbali kutoka ndani ya nje ya nchi.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

APRILI 7,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • AMEUONA Mwenge Songea baada ya miaka 63 ya Uhuru

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru watingisha Manispaa ya Songea,wapitia miradi ya bilioni 1.8

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua jengo la OPD zahanati ya Jimbo katoliki Mvinga

    May 14, 2025
  • MWENGE wa Uhuru wakagua mradi wa jengo la OPD zahanati ya Jimbo Katoliki Mbinga

    May 14, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.