Soko la Mbamba bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma limeteketea Kwa moto usiku wa kuamkia Tarehe 16/11/2024 na kuuunguza vibanda 25 vya soko hilo na mali ambazo zilikuwepo katika vibanda hivyo.
Chanzo cha moto Bado hakijaeleweka.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Mbamba bay Mhe Ajali Hasan, Kila duka lilikuwa na Mali.
Mashuhuda wamesema kwamba majira ya saa 9 usiku waliona moto ukiwa unawaka katika soko hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres magiri,Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya na viongozi mbalimbali wamefika katika katika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole Wananchi wa Mbamba bay
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.