Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Wilaya ya Songea inatarajia kukamilisha ujenzi wa madarasa yote 96 yanayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.9 ifikapo Novemba 30 mwaka huu.
Akizungumza na Menejimenti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Songea,Mheshimiwa Mgema amesema ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari unaendelea vizuri ambapo wanatarajia kumkabidhi madarasa yote Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ifikapo Desemba 10 mwaka huu.
Ameitaja Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwa imepewa shilingi bilioni 1.5 kujenga madarasa 76 ukilinganisha na Halmashauri za Songea ambayo imepewa milioni 200 kujenga madarasa 10 na Madaba pia imepewa shilingi milioni 200 kujenga madarasa 10.
Wilaya ya ya Songea inaundwa na Halmashauri tatu ambazo ni Manispaa ya Songea,Halmashauri ya Madaba na Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mkoa wa Ruvuma umepokea zaidi ya shilingi bilioni tatu kujenga madarasa 156 ya sekondari katika Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.