• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SONGEA mji wenye utajiri wa kihistoria na kishujaa Tanzania

Imewekwa kuanzia tarehe: January 28th, 2020

MJI wa Songea uliopo katika Mkoa wa Ruvuma  ni miongoni mwa maeneo machache hapa nchini ambayo yana hazina kubwa ya utajiri  wa kihistoria  na kishujaa.

Mashujaa kutoka katika Mji wa Songea waliendeleza mapambano dhidi ya ukoloni wa Kijerumani hivyo kuchangia kikamilifu harakati za ukombozi kabla ya kupata uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Jina la Mji wa Songea ni kumbukumbu ya  Nduna Songea Mbano ambaye alikuwa na Ikulu yake katika Mji wa Songea.Mji wa Songea una majengo ya kumbukumbu za  kihistoria mbalimbali yakiwemo makanisa yenye miaka zaidi ya 100.

Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Bartazar Nyamusya anasema historia inaonesha kuwa Mji wa Songea ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani.

“Mji wa Songea uliendelea kukua na kuwa Makao makuu ya  utawala wa Wajerumani katika Wilaya ya Songea,Mji huo ulizinduliwa rasmi kuwa mji wa kihistoria,kishujaa na kiutalii mwaka 2010’’,anasema Nyamusya.

Hata hivyo Nyamusya anabainisha kuwa Mji wa Songea  uliathirika na Vita ya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 na Vita kuu ya pili ya Dunia kati ya mwaka 1939 hadi 1945.

Licha ya Mji huo kuathirika na vita hivyo,uliendelea kuwa Makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa utawala wa  Waingereza katika Tanganyika,baada ya uhuru hadi leo  bado Songea ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma.

Anasema Mji wa Songea una umaarufu wa mashujaa wa Vita vya Majimaji ambapo mashujaa 67 walinyongwa mwaka 1906 kati yao mashujaa 66 walizikwa katika kaburi moja.

Nyamusya anabainisha kuwa Nduna Songea Mbano ambaye alikuwa na umaarufu,alinyongwa na  kuzikwa katika kaburi lake  ambapo makaburi yote yapo katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea.

Mashujaa hao 67 walinyongwa katika eneo lililojengwa Mnara wa Mashujaa wa vita vya Majimaji nyuma ya ukumbi wa Songea ambalo ni kivutio cha aina yake cha utalii katika Mji wa Songea .

Mhifadhi huyo wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji anasema Mkoa wa Ruvuma pia ulitoa mashujaa walioshiriki katika Vita kuu ya pili ya Dunia ambapo mashujaa 270  walishiriki katika vita hiyo kati yao mashujaa watatu walikuwa ni wanawake.

Akizungumzia kuhusu Makumbusho ya Majimaji,Nyamusya anasema yalianzishwa rasmi mwaka 1980 na kusimamiwa na Hayati Dk.Lawrence Gama wakati huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Hata hivyo anasema mchakato wa kuyakabidhi Makumbusho hayo chini ya Shirika la Makumbusho ya Taifa ulianza Mei hadi Novemba 2009 ukisimamiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Christine Ishengoma.

Makumbusho hayo yalikabidhiwa katika Shirika la Makumbusho ya Taifa chini ya sheria ya makumbusho ya Taifa la Tanzania,namba saba ya mwaka 1980 hivyo makumbusho hayo yalipandishwa hadhi na kuwa Makumbusho ya Taifa mwaka 2010.

“Haya ni Makumbusho pekee nchini ambayo imebahatika kuwa na vifaa muhimu katika historia ya Mtanzania ,mchakato uliopo hivi sasa ni Makumbusho hayo kuchukuliwa kuwa ya Kitaifa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili iwe endelevu”,anasisitiza Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa.

Anabainisha zaidi kuwa Mji wa Songea ni miongoni mwa miji michache ambayo ilitoa upinzani mkali katika vita vya Majimaji ambapo katika Makumbusho hayo kuna ushahidi ambao unaonesha moja kwa moja kuwa wazee wa Songea walishiriki kikamilifu katika vita hivyo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.