• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SONGEA tumekamilisha kazi ya Rais Dkt.Samia-DC Mgema

Imewekwa kuanzia tarehe: December 20th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Halmashauri tatu katika Wilaya ya Songea zimekamilisha kwa mafanikio makubwa kazi ya kujenga madarasa 96 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mgema amesema hayo baada ya kukagua madarasa 29 kati ya 76 yaliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

“Sisi Wilaya ya Songea tumekwishafanya kazi tuliotumwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tumeikamilisha kwa mafanikio makubwa “,alisema

na kuongeza kuwa wanafunzi wote watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 watapata mahali pazuri pa kusomea.

Amesema madarasa yote 96 yaliyojengwa Wilaya ya Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9 yamejengwa katika viwango na ubora wa hali ya juu.

Amebainisha zaidi kuwa madarasa yote yamewekewa malumalu,nishati ya umeme,viti na meza pamoja na milango yenye viwango bora inayolingana na thamani ya madarasa.

Amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuleta fedha shilingi bilioni 1.9 katika Wilaya ya Songea ambazo zimejenga madarasa 76 katika Manispaa ya Songea kwa shilingi bilioni 1.5,madarasa kumi katika Halmashauri ya Madaba ambayo yamegharimu sh milioni 200 na madarasa kumi katika Halmashauri  ya Songea ambayo yamegharimu shilingi milioni 200.

Hata hivyo amesema kazi ya ujenzi wa madarasa iliyofanywa katika Wilaya ya Songea inakwenda kujenga taswira katika Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kwa sababu asilimia 80 ya madarasa yote  yaliyopewa fedha za madarasa yapo Wilaya ya Songea.

Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Songea wakiwemo Monica Haule na Frank Komba wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea kero ya vyumba vya madarasa wanafunzi wa shule za sekondari.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Ruvuma imetoa shilingi bilioni 3.2 kujenga madarasa 156 katika shule za sekondari ili kukabiliana na upungufu wa madarasa kwa wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza Januari 2023.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.