RAIS SAMIA ATOA BILIONI 145.7 KUJENGA MRADI MKUBWA WA MAJI SONGEA
SERIKALI inatarajia kuanza kutekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea mkoani Ruvuma unaogharimu shilingi bilioni 145.7.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa amesema hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo kati ya serikali na Mkandarasi unatarajia kufanyika Machi 10,2023 kwenye viwanja vya shule ya msingi Matarawe mjini Songea.
Amesema Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marypriska Mahundi na kwamba Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo ni Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation.
“Mkataba wa ujenzi wa mradi huo ni wa miezi 32 kuanzia Machi 10,2023,kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea kutaleta manufaa ikiwemo SOUWASA kuongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka lita milioni 11.58 kwa siku hadi kufikia lita milioni 42.581 kwa siku hivyo kuwa na uhakika wa kuwahudumia wananchi wapatao 440,794’’,alisisitiza Mhandisi Kibasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.