SERIKALI ,imetenga Sh.bilioni 1.168 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji ya bomba utakaowaondolea adha ya huduma ya maji safi na salama wakazi zaidi ya 12,000 wa kata ya Subira katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Mhandisi wa maji kutoka ofisi ya Meneja wa Mamlaka ya Maji naUsafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) Charles Kitavile.
Kitavile ametaja kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa nyumba mbili za kuhifadhi mashine(pump house) tenki la kuhifadhi maji lita 200,000 na kupeleka umeme kwenye mashine za kusukuma maji.
Kazi nyingine ni kuchimba mitaro na kulaza mabomba umbali wa kilomita 45.5 na hadi sasa kazi zilizofanyika ni ununuzi wa mabomba,kuchimba mitaro urefu wa kilomita 14.5 na utekelezaji wake umefikia asilia 25.
Kitavile amewataka wananchi ,kuhakikisha wanatunza miundombinu ya mradi huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na usaidie kumaliza changamoto ya huduma ya katika maeneo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.