Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) imetambulisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1 katika maeneo ya Sinai na Londoni Manispaa ya Songea.
Mradi huu unalenga kunufaisha wakazi wapatao 5,883 kwa kuboresha miundombinu ya maji na kupunguza adha ya kutafuta maji kwa umbali mrefu.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa SOUWASA, Mhandisi Japhary Yahaya, amesema kuwa mradi huo utajumuisha uchimbaji wa visima viwili, ujenzi wa tanki lenye uwezo wa lita 200,000, pamoja na ujenzi wa nyumba mbili za pampu na mfumo wa kutibu maji.
Amelitaja lengo kuu ni kuhakikisha wakazi wa Sinai na Londoni wanapata huduma bora ya maji safi na salama, hatua inayotarajiwa kuboresha afya na ustawi wa jamii.
Diwani wa Kata ya Lilambo, Yobo Mapunda, ameipongeza SOUWASA kwa juhudi hizi, akisema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka kwani wakazi wa Sinai wamekuwa wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.