Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) mkoani Ruvuma imepewa Tuzo baada ya kushika nafasi ya pili katika utoaji bora wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa mamlaka kubwa zenye wateja zaidi ya 20,000.
Tuzo hiyo imetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji Kazi wa Mamlaka za Maji kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Cheti hicho ni uthibitisho wa jitihada za SOUWASA katika kuhakikisha wananchi wa Songea wanapata huduma bora za maji na usafi wa mazingira.
Mamlaka hiyo imewekeza katika miundombinu na kuimarisha usimamizi wa rasilimali ili kuboresha huduma zake.
Hivi karibuni, SOUWASA imeongeza uwezo wake wa uzalishaji na usambazaji wa maji, hatua iliyochangia mafanikio haya.
Utoaji wa tuzo hizi unalenga kuhamasisha mamlaka nyingine za maji kuboresha huduma kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.