Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imetoa shukrani kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa wawili waliodaiwa kuhusika na wizi wa mita za maji na vifaa vingine vya miundombinu ya maji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA, Mhandisi Patrick Kibasa alisema wizi wa mita za maji umekuwa changamoto kubwa inayosababisha usumbufu kwa wateja.
“Kwa siku tumekuwa tukiibiwa mita zisizopungua saba, na hadi sasa zaidi ya mita 185 zimepotea. Tumeingia gharama ya zaidi ya shilingi milioni 50 kuziba hasara hiyo ili huduma ziendelee,” alisema Kibasa
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Idrisa Mnimi (21) na Ramadhani Athuman Kalumbu (19), wote wakazi wa Songea.
Watuhumiwa hao walikamatwa Aprili 11, 2025, katika Mtaa wa Matarawe, wakiwa na mita 27 za maji, cover meter 8, ball corki 161 na ball valve 77 – vyote vikiwa ni mali ya SOUWASA.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.