• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

STOF yaytaua changamoto ya maji katika shule tatu Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: January 20th, 2025

TAASISI ya Isiyokuwa ya Kiserikali ya St.Teresa Orphans Foundation (STOF) imetoa Zaidi ya shilingi milioni 30 kukarabati majengo ,kununua madawati 25,kukarabati na kuchimba visima vitatu katika shule za msingi tatu Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa STOF nchini Tanzania Moses Nyirenda katika hafla ya kuishukuru STOF iliyofanyika katika shule ya msingi Unangwa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni  Mkurugenzi wa STOF nchini Marekani Teresa Nyirenda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa STOF nchini Tanzania,kati ya fedha hizo,jumla ya shilingi milioni 15 zimetolewa kwa ajili ya kukarabati majengo ya shule ya msingi Unangwa, shilingi 700,000 zimetumika kununua madawati 25 katika shule hiyo na shilingi 600,000 zimetumika kukarabati kisima cha maji.

Nyirenda amebainisha Zaidi kuwa STOF pia imetoa shilingi milioni  15.9 kuchimba visima viwili  vya maji katika shule za msingi Msamala na Mkuzo hivyo kutatua changamoto ya  ukosefu wa maji kwa wanafunzi katika shule hizo na kuzuia magonjwa  mbaimbali ikiwemo ugonjwa wa matumbo.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi katika shule tatu za Unangwa,Msamala na Mkuzo,Mkurugenzi wa STOF nchini Marekani Teresa Nyirenda amewapongeza walimu na Kamati za Ujenzi kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi hiyo iliyofanikisha kupeleka maji katika shule tatu za msingi hivyo kutatua changamoto ya maji kwa wanafunzi katika shule hiyo.

“Unapoona mtoto hajakunywa maji tangu asubuhi,halafu chooni hakuna maji ni kitu ambacho kimenishitua hivyo sio STOF tu bali inatakiwa kuhamasisha hata wadau wengine kupita katika shule za msingi na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo ukosefu  wa maji nimejifunza kitu kikubwa sana kupitia ziara hii’’ Nyirenda,alisisitiza.

Ameahidi kuendelea kusaidia changamoto nyingine zikiwemo ukarabati wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Unangwa ambapo amewapongeza  Kamati ya ujenzi kwa kutumia fedha vizuri za kukarabati majengo ya shule hiyo ambayo yalikuwa chakavu.

Amesema Taasisi binafsi zinawajibu wa kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa kuwa serikali pekee inasimamia miradi mingi na haiwezi kutekeleza huduma zote kwa asilimia 100 hivyo sekta binafsi zina mchango mkubwa.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Msingi Mkuzo Mwanaharusi Msomwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, ameishukuru STOF  kusaidia kuchimba kisima cha maji safi katika shule hiyo, hivyo ameomba ushirikiano kati ya STOF na Serikali uendelee katika masuala mbalimbali.

Nao wanafunzi  katika shule hizo wakizungumza kwa nyakati tofauti,wameishukuru STOF kwa kuwapelekea maji  yanayowawezesha   kupata maji ya kunywa,kupikia,kufanyia usafi na kumwagilia maua katika shule zao hivyo shule kuwa na mazingira ya kuvutia.

Shule ya msingi Msamala ina wanafunzi 810 na  shule ya msingi Mkuzo ina wanafunzi 1400  hivyo kupatikana kwa maji ya uhakika katika shule hizo ni kutatua changamoto nyingi zinazotokana na ukosefu wa maji.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.