• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SUMA JKT yazindua mradi wa shamba la kilimo na mifugo Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: August 19th, 2022

MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Wakili Julius Mtatiro,amezindua mradi  mkubwa wa shamba la kilimo na ufugaji la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) lenye ukubwa wa ekari 1,280 wilayani humo.

Shamba hilo, linasimamiwa na Kampuni Tanzu ya Suma JKT ijulikanayo kama Suma JKT Ports &Services Co. Ltd linatumika kwa kilimo cha zao la korosho,ufugaji wa kuku wa mayai na nyama,mbuzi na ng’ombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba hilo,Mtatiro amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele na Mkurugenzi wa Suma JKT Kanali Petro Ngata kwa kuleta mabadiliko makubwa  ndani ya Jeshi hilo ikiwamo kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Mtatiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya wilaya ya Tunduru, ameitaka Suma JKT kuendelea kupanua wigo wa shughuli zake hasa katika sekta ya kilimo cha korosho kwa kuwa wilaya hiyo  ina maeneo makubwa yanayofaa kwa shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali.

Mtatiro alisema kuwa,katika wilaya  ya Tunduru  kuna hazina kubwa ya ardhi inayofaa kwa kilimo,ambapo hadi sasa ardhi iliyotumika kwa shughuli za kilimo na ufugaji ni asilimia 20 ambapo asilimia 80 zilizobaki, asilimia 60 kwa ajili ya wananchi na  ishirini zimetengwa kwa ajili ya taasisi  mbalimbali za serikali.

Alisema, shamba hilo linalomilikiwa na SUMA JKT lina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 600 ya korosho,hata hivyo uzalishaji huo utafikiwa iwapo  itapandwa miche ya kisasa na kusimamiwa vizuri, badala ya  kutegemea miche ya zamani ambayo uzalishaji wake ni mdogo.

Amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Chiza Marando, kukaa na wataalam wake na kupitia maeneo yote yaliyotengwa kwa kwa ajili ya mpango maalum wa kilimo(Block Farming)na kuwashiriki Suma Jkt ili maeneo hayo yaweze kufanyiwa kazi ili kutimiza  malengo ya Serikali.

Mtatiro,amewaasa wananchi hasa wakulima na wafugaji,kwenda  kujifunza namna  ufugaji  bora na kilimo cha kisasa kwenye shamba hilo ili waweze kupata mafanikio kupitia  sekta hizo,badala ya kuendelea kufuga na kulima kizamani.

Aidha,amewataka watu wanaotaka kuingiza mifugo katika wilaya hiyo kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu  kwa kupeleka mifugo yao kwenye maeneo yaliyotengwa(vitalu) badala ya kuzurura ovyo ili  kuepusha migogoro inayoweza kutokea kati ya wakulima na wafugaji.

“kiasili wananchi wa Tunduru sio wafugaji,lakini kuna watu wanaotoka nje  ya wilaya hiyo na kuingiza idadi kubwa ya mifugo, hata hivyo kutokana na uwekezaji unaofanywa na Suma JKT ni muhimu  kwenda kujifunza namna bora ya ufugaji wa kisasa  na kuepuka kuzurura na makundi makubwa ya mifugo porini”alisema Mtatiro.

Pia,ametoa siku kumi na nne kwa  shirika la umeme Tanesco na Wakala wa usambazaji maji vijijini(Ruwasa) wilayani humo, kupeleka  mpango wao wa kazi ofisini kwake kuhusu maandali ya kupeleka  umeme na maji katika shamba hilo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la uzalishaji mali la Suma JKT Meja Dkt Peter Kulyakwave alisema,shirika la Suma JKT linatekeleza mkakati wake wa kuongeza vyanzo vipya vya mapato na kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.

Alisema, Suma Jkt  imejipanga kujishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwamo kilimo na ufugaji katika shamba hilo kwa kupanda mikorosho mipya,kufuga ng’ombe na kuwanenesha kwa kuwapa chakula na virutubisho vinavyohitajika kabla ya kupelekwa sokoni kuuzwa.

Meja Kulyakwave alisema, shamba  hilo la kilimo na mifugo Tunduru litakuwa sehemu ya mafunzo kwa wananchi hususani wakulima na wafugaji ili waweze kuongeza thamani ya  mazao wanayolima na mifugo na hatimaye kupata bei nzuri wanapofikisha sokoni.

Alieleza kuwa,matarajio ya shirika la uzalishaji  mali la Jeshi la kujenga Taifa (SUMA JKT) kwamba   shughuli zote za kilimo na ufugaji zinazofanyika katika shamba hilo zitaongeza ufanisi katika utendaji wa kampuni kwa kupunguza  baadhi ya changamoto na kuongeza wigo wa mapato.

Amemuagiza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMA JKT Ports & Services, kutoishia kwenye ufugaji na kilimo tu bali  kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao yatakayozalishwa katika shamba hilo na wananchi.

Awali Mkurugenzi Mwendeshaji wa Suma JKT Ports & Services Meja Joseph Marwa alisema, Jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ)lilikabidhi shamba la korosho lililopo katika wilaya ya Tunduru lenye ukubwa wa ekari 2,180 kwa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) mwaka 2017,

Kwa mujibu wa Meja Marwa,lengo ilikuwa ni kulinda eneo hilo na pia kuendesha shughuli za kilimo cha zao maarufu  la korosho ambapo JKT kupitia Shirika la uzalishaji mali la SumaJKT lilianza kukalia eneo hilo mwaka 2019 ambapo kampuni tanzu ya SUMAJKT Ports &Services ilikabidhiwa jukumu  la kusimamia na kuendesha shamba hilo.

Alisema,baada ya kukabidhiwa Kampuni iliweka mpango wa kuliendeleza shamba  ikiwamo kujenga jengo la kukaa vijana,kutunza mikorosho iliyopo,kusafisha shamba kwa awamu na kupanda mikorosho mipya.

Meja Marwa alieleza kuwa,mwaka 2022 JWTZ iliamua kuchukua eneo hilo tena kwa shughuli za kiusalama na kuacha zaidi ya ekari 700 ambapo tayari Suma Jkt lilikuwa limeanza kuziendeleza kwa shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji.

Alisema,mpaka sasa Suma JKT Ports &Services imefanikiwa kusafisha shamba lote,kupana miche mipya 300 ya mikorosho ya muda mfupi,kuhakiki mipaka ya shamba na baada  uhakiki uliyofanywa kwa kushirikiana na ofisi ya Ardhi Wilaya na kamati ya ulinzi na usalama imebaini shamba hilo lina ukubwa wa ekari 2,180.

Aliongeza kuwa,kampuni imeanza kuendesha shughuli  mbalimbali ikiwamo ufugaji  wa kuku wa kienyeji 200 na vifaranga 234,mbuzi 60,ng’ombe wa kunenepesha 20,ulinzi wa mipaka ya eneo na kujenga nyumba  kupokea umeme(Power Hause).

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.