Utafiti umeonesha kuwa, asilimia zaidi ya 96 ya chembe za urithi za binadamu zinafanana na zile za sokwe, pia ubongo wa sokwe na vitendo vyao vinafanana sana na vile vya binadamu.
Profesa Richard wa somo la viumbe kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani anaeleza kuwa, sokwe ni daraja pekee kati ya binadamu na maumbile hivyo ni vema wanyama hao kulindwa kwa nguvu zote.
Mhifadhi wa Hifadhi za Taifa,Noelia Mnyonga anasisitiza tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa Sokwe ni wanyama ambao wanafanana na binadamu katika tabia kwa asilimia 98 na kusisitiza kuwa ndiyo maana wanaitwa sokwe mtu.
“Sokwemtu ni mnyama ambaye alibakiza asilimia mbili tu angeweza kufanana na binadamu kitabia kwa asilimia 100 hali ambayo inamfanya mnyama huyu kutafutwa kwa udi na uvumba baada ya kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha utalii duniani kote’’,anasema Mnyonga.
Mnyonga anasisitiza kuwa sokwe mtu ni mnyama wa ajabu ambaye kwa tabia na matendo hatofautiani sana na binadamu ndiyo maana baadhi ya watu wanamuita binadamu pori.
Sokwe mtu ni mnyama ambaye ni mfano halisi wa binadamu, mnyama huyu anavutia macho ya watalii wengi,ambao wanamiminika hapa nchini katika hifadhi ya Taifa ya Gombe mkoani Kigoms kwenda kuwashangaa wanyama hao adimu na wa aina yake.
Tafiti za kisanyansi zinaonesha kuwa sehemu ya ubongo wa sokwe inafanana na sehemu ya ubongo wa binadamu,hali hiyo ndiyo imesababisha sokwemtu kufanya matendo mengi ambayo yanafanywa na binadamu kwa mfano sokwemtu anaweza kupiga mswaki,kula chakula na kucheza kama binadamu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.