Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma imeandaa warsha itakayowaleta pamoja wadau 300 kujadili huduma zinazotolewa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Akizungumza ofisini kwake, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mbinga Frederick Msae amesema katika warsha hiyo, wananchi watapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu TANESCO na kuelezea changamoto wanazokumbana nazo.
“Wakati wa warsha, wananchi watapata majawabu ya maswali watakayouliza na suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo,” alisema.
Mgeni rasmi katika warsha hiyo itakayofanyika katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) kilichopo Halmashauri ya Mji wa Mbinga anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe Kisare Matiku Makori.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.