MKURUGENZI wa Uzuiaji Rushwa kutoka Makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Sabina Seja amesema Taasisi hiyo katika Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kuokoa fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 740 kutoka katika vyama vya vya ushirika na Benki ya wananchi wa Mbinga.Seja alikuwa anatoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU wilaya ya Namtumbo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu Gorge Mkuchika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.