Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi Milioni 16,736,800 kuanzia Julai hadi Septemba 2024.
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Janeth Haule, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa, mjini Songea.
Janeth amesema kuwa fedha hizo zimeokolewa kwa kudhibiti vitendo vya rushwa na kuwafikisha watuhumiwa mbalimbali mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ameongeza kuwa wamefanikiwa pia kuokoa kiasi cha shilingi Milioni 2,750,000 kutoka katika ujenzi wa jengo la dharura Wilayani Tunduru, ambapo kulitokea ubadhirifu na kusababisha upotevu wa fedha hizo.
Amesema kwa kipindi cha miezi mitatu, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefuatilia miradi 18 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 6,512,542,640 ikijumuisha ujenzi wa madarasa, vyoo, jengo la mama na mtoto, miundombinu ya maji, na barabara.
Amebainisha kuwa miradi miwili kati ya hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni 962,556,000 ilikutwa na mapungufu na hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuondoa mapungufu hayo.
Hata hivyo amesema katika kipindi cha miezi mitatu, TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya rushwa ili kuwahamasisha kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.