Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Ruvuma imebaini mapungufu kwenye miradi 19 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba kwa wanahabari Naibu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule katika ukumbi wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Novemba 16, 2023.
Naibu Kamanda Haule amesema ufatiliaji umefanyika katika sekta ya elimu kwenye Wilaya ya Tunduru ujenzi wa madarasa, jengo la utawala na vyoo katika shule nne zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 911 pia na Wilaya ya Namtumbo ujenzi wa madarasa, jengo la Utawala na vyoo shule nne zenye kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 849.
Katika Wilaya ya Nyasa ujenzi wa madarasa, jengo la Utawala na vyoo shule nne vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 602 pia Wilaya Songea ujenzi wa madarasa, jengo la utawala vyoo na mabweni katika shule 7 zenye thamani ya zaidi bilioni 2.
Naibu kamanda Haule amesema TAKUKURU wamechukuahatua kwenye Baadhi ya miradi ambayo imeonekana na mapungufu uchunguzi unaendelea ukiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo 14 katika shule ya msingi Ngingama Wilaya ya Nyasawenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33 unamapungufu ya fundi kulipwa fedha za uwekaji wa DPC na DPM na ujenzi wa mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua una deni.
“TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi husika tumeendelea na jukumu la kuelimisha umma kwa kuyafikia makundi mbalimbali ya jamii lengo ni kuendelea kuwajengea uelewa wa madhara ya rushwa ili waweze kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa”, amesema Haule.
Katika taarifa yake kamanda Haule amebainisha mapungufukatika sekta ya fedha uchambuzi umejikita kwenye kodi ya zuio na ukataji wa risiti za EFD Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma, baadhi ya mapungufu yamebainika.
TAKUKURU Mkoa katika kipindi tajwa kwa upande wa uchunguzi wamepokea jumla ya malalamiko 38 yanayohusu ruswa 27 yasiyohusu ruswa 11. Malalamiko haya yanatoka katika sekta za ujenzi Fedha ,Ardhi, Nishati, Mahakama, Kazi, Madini Afya, Elimu na Halmashauri.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.