• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAMASHA la kumbukizi ya miaka 114 ya vita ya Majimaji kufanyika Songea kwa siku sita

Imewekwa kuanzia tarehe: February 23rd, 2021

TAMASHA la kumbukizi ya miaka 114 ya vita ya Majimaji linafanyika kwa siku sita katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea.

Mhifadhi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Adson Ndyanabo amesema tamasha hilo linaanza Februari 22 na kilele chake kinatarajiwa kuwa Februari 27 mwaka huu na kwamba katika tamasha hilo wadau watashiriki maonesho ya vyakula vya asili ya Mkoa wa Ruvuma.

Shughuli nyingine zitakazofanyika kwenye tamasha hilo amezitaja kuwa ni kazi za sanaa za mikono,maonesho ya vita ya Majimaji,mavazi ya asili,burudani za ngoma za asili,muziki na kufanyika magwaride ya heshima.

Ndyanabo ameitaja kaulimbiu katika tamasha la mwaka huu kuwa ni Maisha ya wazee wetu fahari yetu na kwamba mgeni rasmi  kenye kilele cha tamasha hilo Februari 27 anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Hata hivyo amesema tamasha hilo linatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro sanjari na kuzindua vilabu vya Historia na uzalendo vilivyoanzishwa katika shule ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Magufuli kuhakikisha vijana mashuleni wanapata elimu ya uzalendo na historia ya nchi kwa ujumla.

Amesema tamasha hilo pia linafanya kongamano la wadau kwa lengo la kupeana elimu,mila na utamaduni wa  Mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia historia ya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,Mhifadhi huyo amesema Makumbusho ya Taifa  ya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea,ni miongoni mwa makumbusho saba ya Shirika la Makumbusho ya Taifa na vituo 91 vya kale vilivyopo nchini.

“Makumbusho ya  Majimaji yalianzishwa na kufunguliwa Julai 6,1980, na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Lawrence Gama,lengo la kuanzisha makumbusho hayo ni kutunza kumbukumbu ya historia ya vita ya Majimaji iliyoanza mwaka 1905 hadi 1907’’,alisisitiza.

 Amesema  Makumbusho hiyo imejengwa katika eneo ambalo mashujaa 67 walizikwa baada ya kunyongwa kikatili na wajerumani.

Amelitaja eneo hilo la mashujaa maarufu kama hero square kuwa kuna makaburi mawili ya mashujaa moja ni la halaiki ambalo wamezikwa mashujaa 66 katika kaburi moja baada ya kunyongwa na serikali ya wakoloni wa kijerumani Februari 27,1906.

Kwa mujibu wa Mhifadhi huyo,kaburi la pili lililopo kwenye makumbusho hayo ni la Jemedari wa wangoni,Nduna (Sub chief) Songea Mbano aliyenyongwa  Machi 2,1906 na kwamba Mji wa Songea umepewa jina la jemedari huyo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Februari 22,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.