Chama Kikuu cha Ushirika wilayaniTunduru (TAMCU) kimetangaza mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua korosho katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, ikiwa ni hatua ya kuongeza thamani ya zao hilo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TAMCU, Marcelino Mrope, wakati wa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 22 uliofanyika katika ukumbi wa Sky Way, mjini Tunduru.
Mrope amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kubangua tani 3,500 za korosho kwa mwaka na kinatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni nne.
Ameeleza kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa kuongeza mnyororo wa thamani wa korosho na kupunguza utegemezi wa kuuza korosho ghafi nje ya nchi
“Uwekezaji huu utaongeza mapato ya ndani kwa wananchi na halmashauri, na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya uchumi wa wilaya yetu,” alisema Mrope.
Mrope aliongeza kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 200 kwa wakazi wa Tunduru, hivyo kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, na kuongeza bei ya korosho kwa wakulima.
Mkulima wa korosho wilayani humo, akiwemo Bi Sharifa Mkwanda na Bw. Lesi Mesi, amefurahishwa na ujenzi wa kiwanda hicho, akisema kitaongeza fursa zaidi za kiuchumi na kuongeza tija katika kilimo cha korosho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.