CHAMA kikuu cha Ushirika katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma(TAMCU LTD) kimeuza jumla ya kilo milioni 106,813,115 ya zao la korosho zenye thamani ya Sh bilioni 310,336,306,090.0 katika kipindi cha miaka minne.
Meneja Mkuu wa Tamcu Imani Kalembo amesema hayo,wakati akitoa taarifa ya hali ya uzalishaji wa zao hilo kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge.
Katika msimu wa kilimo 2016/2017 Chama hicho kimeuza kilo 15,189,913 zenye thamani ya Sh 46,899,462,396.00,mwaka 2017/2018 kimeuza kilo 20,912,569 zenye thamani ya Sh 79,777,589,485.00,mwaka 2018/2019 kilo 18,586,248 zenye thamani ya Sh 61,334,618,400.00.
Kwa mujibu wa Kalembo,mwaka 2019/2020 kilo 24,625,824 zenye thamani ya Sh 65,376,990,905.00 na katika msimu wa 2020/2021 jumla ya kilo 15,410,551 zenye thamani ya Sh 33,088,547,389.00. zimeuzwa.
Aidha, Tamcu kupitia vyama vya msingi kimekusanya na kuuza jumla ya kilo 9,881,714 ya zao la ufuta lililowaingizia wakulima zaidi ya Sh 22,552,420,857.00 huku zao la mbaazi katika msimu wa 2020/2021 kilo zilizouzwa ni 2,206,296 zenye thamani ya Sh 1,306,676,658.00.
Kalembo amesema kuwa, mauzo hayo yamefanyika kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani mfumo ambao wanachama(wakulima) wameukabali kwa kuwa umeleta tija kubwa kwao ikiwemo bei nzuri ya mazao hayo.
Amesema,katika kipindi cha miaka minne iliyopita,Chama Kikuu cha Ushirika Tamcu kimesimamia upatikanaji wa Pembejeo na kutoa mikopo kwa wanachama yenye thamani ya Sh Bilioni 1,670,584,000.00.
Amesema kuwa, mikopo hiyo imewasaidia sana wanachama kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka kilo 15,301,037 mwaka 2017 hadi kufikia kilo 24,625,824 mwaka 2019/2020.
Katika hatua nyingine Kalembo ameeleza kuwa,kupitia Vyama vikuu vya Ushirika hadi kufikia tarehe 24 Julai wameshapokea Viuatilifu vya maji na unga kwa ajili ya kupulizia mikorosho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge amekipongeza Chama hicho kwa kuwa na mikakati mizuri ya kuwasaidia wakulima na kuimarisha zao la Korosho.
Amesema, Serikali haiwezi kutoa Viuatilifu vinavyokidhi kwa kila mmoja kwa muda wote,hivyo ni lazima kuwa na sehemu ya kujazia(kuongeza) mkulima mwenyewe kwa kulima mazao mengine yatakayomuingizia kipato wakati anasubiri msimu wa zao la korosho.
Hata hivyo,ameagiza suala la elimu ya kilimo bora na chenye tija kwa wakulima na kuendelea kuhamasisha wakulima kulima mazao mengine ya biashara kama kama Soya,Alizeti ambayo yatawasaidia kuongeza kipato.
Amesema, serikali itaendelea kutafuta masoko ili kuwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kuendelea kuzalisha na kupitia vyama vya msingi waweze kupata elimu hasa kwa mazao mapya yatakayolimwa na kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na kukomesha kuuza kupitia vipimo haramu vya kangomba.
MWISHO.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.