Chama Kikuu cha Ushirika wa Masoko ya Mazao Tunduru (TAMCU LTD) kimefanya Mkutano Mkuu uliokwenda sanjari na Uchaguzi wa kupata Bodi mpya ya Uongozi wa chama hicho.
Viongozi waliochaguliwa kwenye mkutano huo ni Pamoja na Ndg. Mussa Athumani Manjaule ambaye amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAMCU, Bodi ambayo inaundwa na wajumbe sita.
Mkutano huo ulifanyika mjini Tunduru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa vyama vya ushirika, na wanachama wa TAMCU kutoka vyama vya Ushirika vya Msingi vyote vilivyopo wilayani humo.
Mgeni rasmi kwenye mkutano huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Simon Chacha.
Akizungumza kwenye mkutano huo Chacha amewataka viongozi wapya wa TAMCU kusimamia kwa ufanisi mambo na mikakati waliyoahidi kwa wanachama wao.
Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na wanachama, na akawataka wanachama kuchagua viongozi waadilifu watakaowezesha ushirika kufikia maendeleo endelevu.
“Maendeleo ya Ushirika yanahitaji ushirikiano,uadilifu na uaminifu, hivi vyote vinatakiwa kuanza kutengenezwa na sisi viongozi wenyewe’’,alisema Chacha.
Mwenyekiti mpya akizungumza baada ya kuchaguliwa Ndg. Manjaule ameshukuru wanachama kwa kumwamini tena kuwa kiongozi wao,ambapo ameahidi kutekeleza mikakati yote ya TAMCU kwa lengo la kuimarisha ushirika na kuleta maendeleo kwa wanachama wake.
Mkutano huo pia umeshuhudia uzinduzi wa magari mawili mapya ya mizigo aina ya Scania yaliyonunuliwa na vyama vya ushirika vya msingi vya SAMA AMCOS na NGUVUMALI AMCOS kwa ushirikiano na benki ya CRDB.
Magari hayo yananatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima kutoka vijijini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.