Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limewataka wananchi wa mkoa huo kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme .
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma, Alan Njiro, akizungumza katika kijiji cha Mkurumusi, Kata ya Mpitimbi, Wilaya ya Songea, aliwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu kulinda miundombinu hiyo.
Aliwataka kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na wizi wa nyaya, akisisitiza kuwa madhara yake hayaiathiri TANESCO pekee bali pia jamii kwa ujumla.
Njiro aliwataka wananchi kutoa taarifa za haraka wanapowaona watu wasiofahamika wakishughulika na transfoma.
Alieleza kuwa kutofichua wahalifu kunaweza kusababisha jamii kukosa huduma ya umeme, jambo linaloweza kuathiri shughuli mbalimbali kama biashara, elimu, na afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.