Idadi ya vijiji vya Mkoa wa Ruvuma vinavyopata umeme vimeongezeka hadi kufikia 489 sawa na asilimia 88.3 ya vijiji vyote 554 vya Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Vijiji 65 vilivyobaki vinaendelea kuunganishiwa umeme kupitia Mradi wa REA awamu ya tatu Mzunguko wa Pili kwa gharama ya Shilingi Bilioni 91.24.
Hata hivyo amebainisha kuwa utekelezaji wa Miradi ya kuboresha miundombinu unaendelea kutekelezwa katika miradi 43 kwa gharama ya Zaidi ya shilingi 2.7 na kwamba utekelezaji wa Miradi 22 ya kuongeza miundombinu unafanyika katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Amebainisha Zaidi kuwa Miradi 27 ya matengenezo ya miundombinu inaendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni 2.8.
Mkoa wa Ruvuma umeweza kuwaunganishia umeme wateja 11,512 sawa na asilimia 76.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.