wananchi wa Mkoa wa Ruvuma mnatangaziwa kuwa Uandikishaji wa wapiga kura utafanyika kwa muda wa siku kumi kuanzia tarehe 11 Oktoba, 2024 hadi tarehe 20 Oktoba 2024.
➢ Kwa upande wa vijiji Uandikishaji utafanyika katika kitongoji kwa ajili yauchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji.
➢ Kwa upande wa mitaa uandikishaji utafanyika katika mtaa kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa Kamati ya Mtaa.
Ndugu wananchi ,Uandikishaji wa wapiga kura utafanyika kwenye majengo ya umma na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishaji utafanyika sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.
Ndugu wananchi ,Vituo vya uandikishaji wa wapiga kura vitafunguliwa saa mbili kamili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili kamili jioni.
➢ Vyama vya Siasa vitaruhusiwa kuwekamawakala wao wakati wa uandikishaji wa wapiga kura kwa gharama zao.
➢ Wakati wa uandikishaji wananchi hawataulizwa masuala yanayohusu shughuli zao, uanachama wa chama cha siasa au dini.
Ndugu wananchi,Tarehe 21 Oktoba, 2024 Orodha ya wapiga kura itabandikwa katika vituo vya kujiandikisha na kupiga kura ili kuwezesha wananchi kukagua orodha ya wapiga Kura.
➢ Mkazi aliyejiandikisha kupiga kura atakuwa na haki ya kuweka pingamizi katika muda wa siku saba kuanzia tarehe 21 Oktoba, 2024 hadi tarehe 27 Oktoba,2024.
Ndugu wananchi , Mpiga Kura atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
(a) ni raia wa Tanzania;
(b) ana umri wa miaka 18 au zaidi;
(c) ni mkazi wa kijiji au kitongoji au mtaa ambao Uchaguzi unafanyika;
(d) ana akili timamu; na
(e) awe amejiandikisha kupiga kura katika kitongoji au mtaa au kijiji husika.
Ndugu wananchi .Mpiga kuraatapoteza sifa ya kupiga kura endapo:
(a) hana moja wapo ya sifa zilizoainishwa hapo juu;
(b) Amejiandikisha kupiga kura katika kituo zaidi ya kimoja.
Sifa za Mgombea
➢ Mkazi yeyote wa kijiji au kitongoji au mtaa anaweza kugombea nafasi yoyote katika Uchaguzi endapo:
➢ ni raia wa Tanzania;
➢ ana umri wa miaka 21 au zaidi;
➢ anaweza kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza;
➢ ana shughuli halali ya kumwezesha kuendesha maisha;
➢ ni mwanachama wa chama cha siasa na amedhaminiwa na chama hicho; na
➢ ana akili timamu.
Ndugu wananchi ,Mtu hatakuwa na sifa za kugombea nafasi yoyote katika uchaguziendapo:
➢ amepoteza sifa zilizoainishwa hapo juu
➢ amehukumiwa hukumu ya kifo na Mahakama za Tanzania au anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi sita gerezani;
➢ hajatangaza kuwepo kwa mkataba au maslahi katika kampuni yenye mkataba na kijiji ambacho anataka kugombea;
➢ amepoteza sifa ya kupiga kura; au
➢ ataajiriwa au kuteuliwa katika wadhifa wowote katika Utumishi wa Umma au kuchaguliwa katika nafasi ya udiwani, ubunge, uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.