MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amegawa Sukari tani 11 iliyokamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa makundi maalumu.
Akizungumza katika tukio hilo la ugawaji wa Sukari hiyo amempongeza Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma pamoja na timu yake kwa kazi nzuri yakuhakikisha biashara za magendo zinakamatwa.
’’Mmeendelea kuchapa kazi licha ya haya Mapato Mkoa wa Ruvuma unafanya vizuri kipekee niwapongeze sana’’.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Ruvuma Amina Ndumbogani amesema mwaka jana wali fanikiwa kukamata sukari iliyoagizwa nchini kwa njia ya magendo.
Amesema hii ni kutokana na doria za kila mara zinazofanywa na ofisi ya TRA Mkoani Ruvuma za kuzuia magendo zinazoendeshwa chini ya kitengo cha forodha na ushuru wa bidhaa.
‘’Kiasi cha mifuko 550 ambayo ni sawa na Tani 11 zikiwa zinaingizwa nchini mwetu kinyume cha sheria na taratibu zetu za forodha’’.
Hata hivyo Ndumbogani amesema ofisi ya Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato imetoa ruksa ya kugawa sukari hiyo kwa Makundi Maalumu ikiwa chini ya Mkuu wa Mkoa.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato ametoa Wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuacha kufanya biashara ya kuingiza bidhaa nchini bila kufuata sheria na taratibu za forodha na ushuru wa bidhaa ya mwaka 2004 na 2010 chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema katika tukio hilo amesema kunahitajika kuimarisha Doria katika mipaka ili kuhakikisha biashara za magendo zinakomeshwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Desemba 6,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.