• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TANI zaidi ya 1500 za mbaazi zanunuliwa Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: September 5th, 2022

TANI zaidi 1593 za zao la mbaazi zimeweza kununuliwa katika mnada wa kwanza wa mbaazi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Meneja wa Ghala Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) Sarah Chorwa amesema ununuzi huo umefanyika kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye vyama vya ushirika vya msingi.

Hata hivyo amesema mnada wa pili unatarajia kufanyika Alhamis wiki hii ambapo hadi sasa tayari wana tani 135 na upokeaji wa mbaazi bado unaendelea.

“tunatarajia hadi mwisho wa msimu huu kufikisha tani zaidi ya 5,000 za mbaazi’’alisema Chorwa.

Amesema katika msimu  huu kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani waliweza kununua zao la ufuta zaidi ya tani 2500.

Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mzuri na wakulima wengi wameukubali na kwamba unawarahisishia wanunuzi kupata mzigo kwa pamoja.

Amesema mfumo huo unawanufaisha watu mbalimbali wakiwemo wasafirishaji,makuli na akinamama lishe na kwamba serikali inapata mapato yake kwa urahisi.Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumzia Mfumo huo amesema mfumo wa stakabadhi ndiyo mkombozi wa wakulima kwa sababu unatoa soko la uhakika kwa wakulima.

Hata hivyo Amesema kuna siasa zinapigwa chini chini kuonekana kama mfumo huo haufai .

Amesema serikali ya Mkoa imefanya mawasiliano na Wizara ya kilimo kupata kibali cha kuuza mbaazi kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo tayari mnada wa kwanza umefanyika wilayani Tunduru na wananchi wengi wamejitokeza na wanafaidika.

Ametahadharisha kuwa wafanyabiashara ambao hawawatakii mema wakulima ndiyo wanaopambana kuhakikisha Mfumo huo unakufa ili wao waweze kufaidika.

Amesisitiza kuwa wafanya biashara hao walikuwa wanawaibia wakulima kupitia pembejeo za kilimo ambapo hivi sasa Mheshimiwa Rais ametoa ruzuku ya mbolea kutoka shilingi 130,000 kwa mfuko ambayo imeshuka kati ya shilingi 70,000 hadi 50,000 kwa mfuko kutegemea na aina ya mbolea.

“Nawashauri  na kuwasisitiza kuwa Mfumo wa stakabadhi ghalani una faida kubwa zaidi kuliko uuzaji holela “,alisema RC Thomas.

Nao wakulima katika wilaya za Tunduru,Songea na Namtumbo wametoa rai kwa serikali kuhakikisha mfumo unakuwa endelevu kutokana na faida nyingi wanazopata wakulima.

Ahmed Salehe Mkulima wa Ligunga Tunduru Amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeongeza Usalama wa fedha za mkulima na umechangia kutoa ajira katika makundi mbalimbali.

Amesema Mfumo huo unatoa bei sawa kwa wakulima wote ambapo ametolea mfano kwenye mnada wa zao la mbaazi mkulima amenunua kwa kilo shilingi 800.

Sophia Mambo mkulima wa Mbesa Tunduru amesema kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima wanapata bei kubwa ya mazao wakati kwenye Mfumo holela wakulima wananyonywa kwa kuuza mazao bei ya chini.

Basilius Komba Mkulima wa Ndongosi Songea amesema wakulima walikuwa wanateseka kwenye Mfumo holela ambapo Mfumo wa stakabadhi ghalani umekuwa rafiki kwa mkulima na wanapata faida kubwa.

Mazao ambayo yanauzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani mkoani Ruvuma ni ufuta,soya,mbaazi,korosho na kahawa.

Imeandikwa na Albano Midelo,Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.