Mrakibu Msaidizi wa Polisi (RTO) Mkoa wa Ruvuma Issa Millanzi ameziomba mamlaka za Barabara (TANROADS) na (TARURA) kufanya marekebisho ya barabara zenye kiwango cha vumbi na changarawe yafanyike mapema kabla ya mvua.
Amesema kulingana na tafiti zinazoonesha kuwepo kwa vyanzo mbalimbali vya ajali za barabarani, ubovu wa barabara ni miongoni mwa sababu zinazosababisha uwepo wa ajali.
Milanzi ameyasema hayo wakati anazungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma ambacho kimefanyika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Millanzi ameshauri kuwekwa alama za barabarani kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea ili kumpa tahadhari mtumiaji wa barabara .
“Maeneo yenye Zebra Crossing na mikusanyiko ya watu yawekewe matuta ili kupunguza mwendo kasi kwa madereva wengi wasio tii sheria bila shuruti na kutoa kipaumbele kwa watembea kwa miguu”, amesema Millanzi.
Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Roman Mbukwini amesema barabara za mkoa zenye lami nzuri ni asilimia 98, barabara za changarawe , udongo ni asilimia 17.7 na asilimia 5.07 ni barabara mbaya.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Wahabu Nyamzungu, amesema jumla ya km 4,268.866 za mtandao wa barabara Mkoa wa Ruvuma zinasimamiwa na TARURA sawa na asilimia 59.73.
Ameishuru Serikali kuwaongezea fedha TARURA kutoka kiasi cha fedha bilioni 7 hadi bilioni 27 kwa mwaka 2022/2023.
Imeandikwa na Farida Baruti kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.