WAKALA wa barabara Tanzania(TANROADS) mkoa wa Ruvuma,imeanza kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara katika mto Namiungo wilayani Tunduru ambayo iliharibiwa na mvua na kutishia kukata mawasiliano kati ya mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine ya Lindi,Mtwara,Pwani na Dar es slaam.
Msimamizi wa matengenezo kutoka Tanroads mkoani humo Mhandisi Godfrey Robbi alisema,tarehe 29 Februari mwaka huu mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa tatu ilisababisha maji kuvuka juu ya daraja na kupelekea upande mmoja wa daraja hilo kukatika na miundombinu yake kusombwa na maji.
Alisema,kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kiuchumi hasa usafirishaji wa makaa ya mawe,wamelazimika kufanya matengenezo ya haraka ili kuruhusu shughuli za usafiri,usafirishaji na kiuchumi ziweze kuendelea kama kawaida.
Aidha alisema,wanaendelea kufanya matengenezo madogo kwenye maeneo mengine ya barabara hiyo ikiwemo eneo la Matemanga-Ligunga na Majala ambayo imeharibika vibaya ili kuwezesha watumiaji wake kupita kwa urahisi.
Robbi,amewataka wananchi hasa madereva kuzingatia alama zilizowekwa katika eneo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea na wananchi kuacha ya kufanya shughuli za kibidamu ikiwemo kilimo ndani ya hifadhi ya barabara, kwani wanaweza kupata hasara pindi maeneo hayo yanapohitaji kupitisha vifaa vinavyotumika kwenye matengenezo ya barabara.
Naye Mhandisi wa kampuni ya Ovans Contructions Ltd inayofanya matengenezo ya daraja hilo Azimio Mwapongo alisema, kazi inayofanyika katika eneo hilo ni kurudisha miundombinu yote iliyosombwa na maji.
Alisema,wameanza kujaza mawe kabla ya kumwaga zege ili kuunganisha zege na lami kwa ajili ya kuzuia maji kupenya kwenye tuta la barabara na kurekebisha baadhi ya alama nyingine zilizoharibika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.