Serikali imepokea rasmi shule mpya ya sekondari Lovund iliyojengwa na Mradi wa Tanzania Project katika Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya shule hiyo, huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alipongeza Mradi wa Tanzania Project kwa kujenga shule hiyo, akisema imeondoa changamoto ya wanafunzi kutembea zaidi ya kilometa saba kufuata elimu.
Alitoa wito kwa walimu, wazazi na wanafunzi kuitunza miundombinu ya shule ili kuwezesha utoaji wa elimu bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Mratibu wa Mradi huo, Mwl. Dennis Katumbi, alieleza kuwa ujenzi unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.2, ambapo hadi sasa shilingi milioni 998 zimetumika,.
Amesema utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 87 ya miundombinu ambapo serikali kuu imechangia shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha bweni la wasichana.
Amesema awamu ya nne ya mradi inahusisha ujenzi wa maktaba, nyumba moja ya walimu, kichomea taka na uzio wa shule.
Mbunge wa Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, aliipongeza Tanzania Project kwa mchango wake katika sekta ya elimu na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanatumia fursa hiyo ya elimu.
Mkurugenzi wa mradi huo, Hanne, aliwashukuru wafadhili kutoka Norway na kusisitiza kuwa elimu ni ufunguo wa maendeleo kwa jamii.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa aliahidi majengo hayo yatatunzwa ili elimu bora itolewe kwa wanafunzi.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway aliahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Norway kwa maendeleo ya sekta ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.