• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA ilivyounganisha wilaya za Nyasa na Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: March 10th, 2023

BAADHI ya wananchi wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamesema,miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,imewafanyia mambo makubwa na kuitendea haki wilaya hiyo kwa  kutatua kero na changamoto nyingi zilizokuwepo tangu nchi ilipopata Uhuru mwaka 1961.

Wamesema,moja kati ya kero kubwa  ilikuwa barabara za kuunganisha kijiji kimoja hadi kingine,lakini sasa kero hiyo haipo kufuatia serikali  ya awamu  ya sita  kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura) kutoboa na kufanya matengenezo ya barabara nyingi wilayani Nyasa.

John Mkomola mkazi wa kijiji cha Ngumbo amesema, Rais serikali  ya awamu ya sita imewatendea haki kwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kuboresha barabara zilizorahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali.

Mkomola ambaye ni Katibu wa CHADEMA kata ya Ngumbo wilayani humo,emeipongeza serikali kwa kazi kubwa iliyofanya ya kuimarisha na kuboresha barabara ambazo zimewezesha wananchi na vijiji vingi kufikiwa na huduma za kijamii.

Amesema,baadhi ya maeneo katika wilaya ya Nyasa hayakuweza kufikiwa na baadhi ya huduma  za kijamii kwa kukosa barabara, hivyo kusababisha maisha yao kuwa magumu licha ya wilaya hiyo kuwa na rasimilia kubwa ya ardhi na ziwa Nyasa lenye samaki wengi.

Adolat Kapinga mkazi wa kijiji cha Lugali amesema,awali barabara ya Ngumbo-Litoho inayounganisha wilaya ya Nyasa na Mbinga haikuweza kupitika kwa urahisi kutokana na ubovu hasa mashimo mengi na makubwa katikati ya barabara na utelezi wakati wa kiangazi.

Hata hivyo ameeleza kuwa,katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Samia barabara hiyo imeimarika na kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hizo mbili ambao sasa wanatembea kifua mbele na kufaidi matunda ya serikali yao.

Ameipongeza serikali kwa  kuendelea kujenga na kuboresha barabara na kurudisha mawasiliano katika maeneo mengi ya wilaya hiyo ambayo hapo awali hayakufikika kwa urahisi kutokana na ubovu wa barabara.

“lazima tukubali tangu Rais Dkt Samia alipoingia madaraka miaka miwili sasa tunaona mabadiliko mengi na makubwa katika wilaya yetu,barabara hii haikuweza kupitika kirahisi, lakini sasa serikali kupitia Tarura imeiboresha na kuunganisha mawasiliano kati ya wilaya ya Mbinga na Nyasa”amesema Kapinga.

Kwa upande wake meneja wa TARURA wilaya ya Nyasa Thomas Kitusi amesema,barabara ya Ngumbo –Litoho yenye urefu wa km 6.59 ilitengewa jumla ya shilingi milioni 84 kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kiwango cha chanagarawe.

Aidha amesema,katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya barabara ikilinganisha na miaka ya nyuma.

Kitusi ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha nyingi zinazotokana na tozo na fedha za mfuko wa Jimbo ambazo zimewezesha Tarura kufanya matengenezo ya barabara nyingi za vijijini ambazo zimeleta mabadiliko makubwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.