• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA kung'arisha mji wa Tunduru kwenye mtandao wa barabara

Imewekwa kuanzia tarehe: March 23rd, 2023

WAKALA wa barabara za mijini na vijijini Tanzania(TARURA)umeanza ujenzi wa barabara ya Islamic Center-Mkunguni kata ya Masonya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma yenye urefu wa kilomita 1.7 kwa kiwango cha lami.

Ujenzi wa barabara hiyo,utasaidia kurudisha mawasiliano kwa wakazi wa mitaa ya Mkunguni na Misufini kwenda maeneo, kufuatia kuharibika kwa barabara za awali kutokana na mvua za masika zilizonyesha mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu.

Kaimu Meneja wa TARURA wilayani Tunduru Mhandisi Msolwa Julius amesema,mradi huo ni wa mwaka 2022/2023 wenye lengo la kuboresha mji wa Tunduru kwa barabara za lami ambapo utaigharimu serikali Shilingi milioni 769.

Msolwa alitaja muda wa ujenzi  barabara hiyo ni siku 120,na imeanza kujengwa mwezi Januari na inatarajiwa kukamilika mwezi April mwaka huu na inatekelezwa na mkandarasi M/S Luke Associate Ltd chini ya usimamizi wa TARURA.

Amesema,kwa sasa kazi inazofanyika ni kutengeneza(kuseti) barabara yenyewe kabla ya kuweka vifusi na hatimaye kumwaga tabaka la lami kazi ambayo inayoendelea vizuri.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tunduru  Mheshimiwa Said Bwanali,amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kimkakati katika wilaya hiyo ikiwemo barabara hiyo na barabara ya Bias-Ikulu ndogo zinazojengwa kwa kiwango cha lami kuzingatia ubora,viwango na kukamilisha kwa wakati.

“barabara hizi  za lami na zile zinazojengwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya yetu ya Tunduru tunataka zikamilike kwa muda uliopangwa,dhamira ya serikali yetu ya awamu ya sit ani kusogeza huduma kwa wananchi na siyo vinginevyo”alisema Bwanali.

Bwanali ambaye ni diwani wa Masonya,ameishukuru serikali kwa kuendelea kuitengea fedha Tarura kwa ajili ya kujenga barabara za lami katika mji wa Tunduru na kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Alisema wilaya ya Tunduru ni kongwe hapa nchini, na maendeleo yanayofanyika sasa walizoea kuyaona katika mikoa mingine hapa,lakini tangu serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani miaka miwili imefanya mambo mengi na mazuri ya maendeleo ambayo yamebadilisha muonekano  na maisha ya wakazi wa Tunduru.

Alisema,barabara ya Islamic Center-Mkunguni ilikuwa haipitiki kirahisi  kutokana na kuharibika vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na ameipongeza Tarura kwa kazi nzuri ya kutekeleza na kusimamia ujenzi wa barabara  katika wilaya hiyo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.