• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA Mbinga yaanza matengenezo ya barabara mbovu

Imewekwa kuanzia tarehe: March 9th, 2023

SERIKALI kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura)wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,imeanza kazi ya kurejesha miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua za masika katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Miongoni mwa barabara zilizoharibiwa na baadhi ya madaraja yake kusombwa na maji ni Barabara ya Mapera-Mikalanga -Ilela na Mitawa ambayo ilijifunga kutokana na kuharibika vibaya kwa kuwa na mashimo makubwa yaliyosababishwa na mvua za masika.

Meneja wa Tarura wilayani Mbinga Mhandisi Oscar Mussa amesema,serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 672 kurejesha tena miundombinu hiyo ili wananchi waweze kuendelea kuzitumia barabara hizo kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema,barabara hizo ziliharibika kutokana na mvua kubwa za masika zilizonyesha kuanzia mwezi Februari  hadi mwezi Disemba mwaka jana, ambapo pia kalavati moja na madaraja manne yaliharibika na wameanza kuyajenga  upya ili kurudisha mawasiliano katika maeneo hayo.

Alitaja gharama ya kurejesha upya miundombinu hiyo ni shilingi 672  ambazo zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo,na kuwaomba wananchi wawe wavumilivu wakati huu ambao serikali iko kazini.

Richard Milinga mkazi wa kijiji cha Ilela wilayani humo,ameishukuru serikali kwa  kuanza kufanya matengenezo ya barabara hizo,kwani zilikuwa mbaya na  kusababisha shughuli zao za kujiingizia kipato kusimama.

Milinga alisema baada ya kuharibika kwa barabara hizo,walikuwa kwenye wakati mgumu kwa kuwa hakuna usafiri wowote wa chombo cha moto iliyofika katika maeneo yao,badala yake walilazimika kutembea kwa miguu kutoka Ilela kwenda maeneo mengine kufuata huduma za kijamii.

Ameipongeza wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura)kwa kuchukua hatua za haraka kuanza matengenezo ya barabara hizo ambazo ni nguzo kuu ya kiuchumi.

Alisema,ukarabati huo utakapokamilika utawawezesha kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali zilizosimama takribani mwaka mmoja tangu miundombinu ya barabara  ilipoharibika.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.