WAKALA wa barabara za mijini na vijijini(TARURA)wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,kwa mwaka wa fedha 2023/2024,umepokea Sh.bilioni 2.434 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara wilayani humo.
Meneja wa TARURA wilaya ya Nyasa Mhandisi Thomas Kitusi amesema ,kati ya fedha hizo Sh. milioni 934 zinatoka mfuko wa barabara,Sh.milioni 500 za mfuko wa Jimbo na Sh.bilioni moja fedha za tozo na zitatumika kujenga barabara za lami za mitaa na barabara katika mji wa Mbambabay.
Amesema wamedhamiria kila mwaka kuhakikisha wanajenga angalau barabara ya kilomita moja ya lami katika mji wa Mbambabay na walianza mpango huo tangu mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo walijenga barabara moja ya lami na kufunga taa.
Hata hivyo amesema ,ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Mbambabay unalenga kuboresha mji huo maarufu kwa shughuli za utalii ili kuvutia shughuli za utalii na uwekezaji.
Kitusi,ameishukuru serikali ya awamu ya Sita kwa kuiongezea fedha TARURA kwa ajili ya ujenzi na kuboresha miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo ambazo zimewezesha kuimarika kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja,wilaya na mkoa wa Ruvuma wenye utajiri mkubwa wa rasilimali.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Mbambabay wameipongeza serikali ya awamu ya sita kuanza ujenzi wa barabara za lami za mitaa zinazokwenda kuhamasisha na kuchochea shughuli za kiuchumi hasa utalii katika wilaya hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.