TARURA Mkoa wa Ruvuma imeingia mikataba 41 ya matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makalavati inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 11 katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema mikataba hiyo inatekelezwa katika kipindi cha miezi sita kuanzia Septemba 2023 hadi Machi 2024.
Amesema Mkoa wa Ruvuma umetengewa bajeti ya zaidi ya shilingi 22 kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.
Kulingana na Meneja huyo wa Mkoa, Manispaa ya Songea imepangiwa kilometa 513.65, Wilaya ya Songea kilometa 1057.24, Halmashari ya Madaba kilometa 629.69,Wilaya ya Namtumbo kilometa 975.25, Mbinga mji kilometa 1063.51,Mbinga vijijini kilometa 973.340, Wilaya ya Nyasa kilometa 729.91 na Tunduru kilometa 1203.61.
Hata hivyo amesema Miradi mbalimbali ya barabara iliyotekelezwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 na inaendelea kufanyiwa ukarabati katika mwaka wa fedha 2023/2024.
“Natoa wito kwa wakandarasi ambao wanaenda kutekeleza kazi za ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa mwaka 2023/224 kufanya kazi kadri ya mikataba inavyoelekeza na kumaliza kazi kwa wakati’’,alisisitiza Nyamzungu.
Amezitaja baadhi changamoto zinazowakabili kuwa ni magari yenye uzito mkubwa kupita kwenye barabara zilizo chini ya wakala na kusababisha uharibifu mkubwa wa barabara na miundmbinu yake.
Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni wananchi kuendesha shughuli za kilimo katika maeneo ya hifadhi ya barabara pamoja na kupitisha mifugo yao.
Ili kukabiliana na changamoto hizo amesema, TARURA ina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kupima uzito wa magari katika barabara zake na kampeni maalum za ukamataji wa magari yanayozidisha uzito na ujazo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.