• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA wakamilisha ujenzi darala la Libango Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: March 8th, 2023

WANANCHI  wa kijiji cha Libango katika Halmashauri ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma,wameishukuru wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura),kujenga daraja la kudumu linalounganisha kijiji hicho na mji wa Namtumbo.

Wamesema,daraja hilo limemaliza mateso waliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuvuka kwenye maji baada ya daraja la zamani  lililojengwa kwa vyuma na serikali ya awamu ya pili kusombwa mwaka mmoja uliopita.

Imani Mtotomwema ameeleza kuwa,kukamilika kwa ujenzi  wa daraja hilo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji cha Libango na vijiji vingine vya kata ya Namtumbo mjini ambao watalitumia kwenye shughuli zao za uzalishaji mali.

 “tunaishukuru sana serikali ya Rais  Samia kwa ujenzi wa daraja hili maana ndiyo kilikuwa kilio chetu cha muda mrefu kwa sababu wananchi wote wa Libango mahitaji yetu yote tunapata Namtumbo mjini”alisema.

Aidha alisema kuwa, kukosekana kwa daraja katika eneo hilo ilipelekea maisha yao kuwa magumu kwani hawakuweza kuvuka mto Luegu wenye maji mengi kwenda maeneo mengine kupata mahitaji na huduma za kijamii.

Alisema wananchi wengi wa Libango ni wakulima,lakini walishindwa kusafirisha mazao yao kwenda sokoni,hali iliyosababisha umaskini na gharama za maisha kuwa juu.

Adinan Sadik mkazi wa Namtumbo alisema,wananchi wa kijiji cha Libango walishindwa kupata huduma za kijamii kutokana na kukosekana kwa mawasiliano baada ya daraja hilo kusombwa na maji ambapo baadhi ya akina mama wajawazito kushindwa kufika katika vituo vya kutolea huduma kwa wakati.

Mfaume Katondo dereva wa bajaji alisema,daraja hilo limerahisisha kuzifikia huduma  mbalimbali za kijamii na kufungua fursa za kiuchumi kwa wakulima ambao watapeleka mazao  moja kwa moja sokoni kuuza mazao yao ,badala ya wanunuzi  kununua mazao shambani kwa bei ndogo.

“tumefarijika sana kuona ujenzi wa daraja hili umekamilika,daraja hili linakwenda kutatua matatizo yote ya hapo awali ambayo yalikuwa yakitukabili,sasa Libango inakwenda kufunguka”alisema Katondo.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Namtumbo Fabian Lugalaba alisema,ujenzi wa daraja la Libango umefanyika kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza ilikuwa ni usanifu na awamu ya pili ni ujenzi wa daraja lenyewe lenye upana wa mita 30.

Alieleza, katika awamu ya tatu itahusisha ujenzi wa box kalavati ndogo ili kuruhusu maji kupita upande mwingine,kujaza udongo na kufanya matengenezo ya barabara ya Namtumbo –Libango yenye urefu wa kilomita 14 kwa kiwango cha changarawe.

Lugalaba alitaja gharama za ujenzi wa mradi huo ni shilingi bilioni 1,390 kati ya hizo shilingi milioni 890 ni za ujenzi wa daraja na shilingi milioni 500  zitatumika kufanya matengenezo ya barabara.

Kwa mujibu wa Lugalaba,wakala wa barabara Tanzania(Tarura) wilaya ya Namtumbo,unaendelea na mpango wake wa kufungua barabara ili kufika kusiko fikika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili kuboresha na kuharakisha  upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.